Psalms 130

Kuomba Msaada

Wimbo wa kwenda juu.

1 aKutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2 bEe Bwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.

3 cKama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4 dLakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.

5 eNamngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6 fNafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.

7 gEe Israeli, mtumaini Bwana,
maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8 hYeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka dhambi zao zote.
Copyright information for SwhNEN